Ilikuwa ni sekunde, dakika, saa, miezi hadi leo ni mwaka mmoja tangu umetuacha Baba yetu mpendwa MZEE IDDY BELLOH. 

Ni vigumu sana kuamini, umetuachia simanzi ambayo sio rahisi kusahau. Unakumbukwa sana na mkeo Sara Belloh, watoto wako Aysha, Muhojo, Silla, Kurwa, Doto na Luluh, wajukuu zako Tareq, Kisura(Hadya), Iddy, Queen, Kelvin, Zuhura(Zuu), Livingstone (Efatha), Junior (Belloh), Shiraz, Bryton, Miquel (Chifu) na Mussa.  Wakwe zako wote pamoja na ndugu zako Hamis Kilomoni, Mzee Issa, Shangazi yetu Titi Belloh na wapwa zako wote.  

Ulikuwa Mume muadilifu, Baba mwenye makuzi mwema, kaka mwenye busara na babu mwenye upendo wa dhati. Sisi watoto wako tunaahidi kuendeleza maadili, upendo, ushirikiano na yote ambayo umekuwa ukituelekeza kwa ajili ya maisha ya hapa Duniani.  

Tunaamini kwamba Mwenyezi Mungu amekupumzisha mahali pema.

AMIN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...