Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na Jeshi la Polisdi Nnchi zima kupambana na watu watakaovunja sheria ya usafirishaji wa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Nchini limewatahadharisha madereva  watakaozidisha  idadi ya abiria kuliko uwezo wa chombo cha usafari kwani ni kosa kisheria na watakaozidisha abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri watachukuliwa hatua za kisheria.

Operesheni hiyo inaanza leo baada ya tamko la Jeshi la Polisi na kuanza kutekeleza kwa wale wote wataobeba abiria wengi tofauti na uwezo wa basi, watachukuliwa hatua madereva wa daladala,mabasi ya mikoani pamoja na magari aina ya Noah.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kuwa Jeshi la polisi linaanza operesheni ambayo ni endelevu na kuwataka watu wafuate sharia ya ubebaji wa abiria.

Advera amesema kuwa katika kipindi hiki cha siku kuu Jeshi la polisi limejipanga katika kuwadhibiti waendesha bodaboda kwa wataopandisha watu zaidi  ya wawili (mishikaki) kukiona cha mtema kuni kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.

Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika msimu wa sikukuu na uimarishaji wa ulinzi wa watu na mali zao na maisha yaweze kuendelea baada ya sikukuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. NATAMANI PIA WAWEKE NA UTARATIBU WA ABIRIA KUKAA KWENYE FOLENI ISPOKUWA KWA WAZEE NA WANAOHITAJI HUDUMA MAALUMU KAMA WAJAWAZITO NA WALEMAVU.

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...hiyo sheria mpaka daladala za bongo au vp sijaelewa hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...