Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam kinatarajia kuanza kuwajengea uwezo wajasiriamali wa viwanda vidogo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuiendeleza sekta hiyo na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo. 
Kaimu Makamu wa Chuo hicho, Profesa Josephat Itika alisema wakati wa mahafali ya 14 kuwa kwa sasa Kampasi hiyo inaandaa miradi mbalimbali ya ushauri na kozi fupi kwa kushirikiana na chuo cha Stellenbosch cha Afrika Kusini tayari kuanza kwa mpango huo mwakani.
 Alisema pia kampasi itashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuendeleza Viwanda (UNIDO) kutoa mchango wake kwa jamii na serikali katika kuimarisha viwanda hivyo viweze kuzalisha, kuongeza thamani na kutoa ajira. 
 Katika mahafali hayo, Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mkuu mstafu, Barbabas Samatta aliwatunuku shahada mbalimbali za uzamili wahitimu na kutoa zawadi kwa wahadhiri waliofanya tafiti na kutoa machapisho mbalimbali kwa ajili ya kufundishia. Pia wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao walitambuliwa. 
 “Tunafanya hivi ili kama moja ya njia za kutekleza sera ya taifa ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025,” alisema. 
 Alifafanua kwamba mpango huo utafuata miongozo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuwataka wataalamu katika vyuo watumie taaluma zao kubuni miradi inayolenga kulikomboa taifa. Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Ganka Nyamsogoro alisema chuo hicho kinahuisha mitaala yake mara kwa mara ili kukidhi mahitaji ya nchi na dunia. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, 
Profesa Daniel Mkude aliwataka wahitimu kuziendeleza taaluma walizopata kwa kusoma zaidi vitabu na makala mbalimbali kwa ajili ya kupata maarifa na kutoa mchango kwa jamii na taifa. 
 “Kuhitimu masomo siyo mwisho wa kujifunza, jengeni tabia ya kujifunza zaidi na zaidi, taifa linawategemea katika kuleta maendeleo,” alisema. 
 Aliipongeza kampasi hiyo kwa jitihada inazofanya za kutoa elimu na mikakati yake ya kupanua miundombinu ili kuzidi kutoa fursa kwa watanzania kupata elimu ya juu. 
 Jumla ya wahitimu 883 walitunukiwa shahada za uzamili. Kati ya wahitimu hao, wanaume walikuwa 455 sawa na asilimia 51.5 na wanawake 428 sawa na asilimia 48.5.
 Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam wakifurahia kuhitimu masomo yao wakati wa mahafali ya 14 yaliyofanyika Julius Nyerere International Convention Center jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam wakifurahia kuhitimu masomo yao wakati wa mahafali ya 14 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Josephat Itika akiongea wakati wa mahafali ya 14 ya chuo hicho yaliyofanyika Julius Nyerere International Convention Center jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...