Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa Naibu Kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia) akiwa na wenzake aliyekuwa Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya na Bulton Mponezya wakiwa katika Mahakama Kuu Tanzania jijini Dar es Salaam leo wakisomewa shtaka linalowakikabili la makosa ya jinai na uhujumu uchumi.
Watuhumiwa watatu wa uhujumu uchumi wakisindikizwa na Polisi wakitoka mahama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kupewa dhamana. Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Serikali mmechukua jukumu kufukuza na kusimamisha watu kazi. Mfano hapo TPA,tangia waziri mkuu katimua watendaji wakuu, walikaimu/chukua hizi nafasi hadi leo wanajifunza kazi. Matokeo yake macontainer yanaanza kurundikana bandarini na bandari kavu. System zao hazisomi au hazioni containers ndio sababu wanatupa sisi ma agents, but mbona before zilikuwa zinasoma? Wateja wanaanza kutuma mizigo via Mombasa na serikali itakosa mapato bado. Nashauri waziri mkuu arudi hapa bandarini tunaathirika
ReplyDeleteHilo nalo neno wanatakiwa waliangalie kwa jicho la pili maana hali imeshakuwa mbaya bandarini kwa makontena utanzania kumekuwa jalalani.
ReplyDeleteBora serikali "ikose mapato" for now kuliko ile style iliyokuwa ndio kamchezo, 2500 containers?! something had to be done.
ReplyDelete---system zao hazisomi au hazioni containers ndio sababu wanatupa sisi ma agents, but mbona before zilikuwa zinasoma?---
"Zilikuwa zinasoma" matokeo yake wote tumeyaona. Madudu.
From 54 containers to 349 containers to 2480 containers! wayapeleke tu huko Mombasa tusafishe nyumba kwanza
Wakati wa kutumbua majipu lazima kipindi cha mpito kiwe na purukushani kama hizo, ni vizuri wahusika wakaona wata-manage vipi kipindi hiki cha mpito!!
ReplyDelete