Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO
Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam “vibro cholera”. Chanzo cha kikubwa cha ugonjwa huu huletwa na vimelea vilivyomo kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu.
Kwa miaka mingi sasa wananchi wa Tanzania tumekumbwa na magonjwa ya aina mbalimbali ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu ambao umeenea kwa kasi kubwa sana kutokana na kuwepo kwa mazingira hatarishi yanayochochea mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa mwaka 2015 ugonjwa wa kipindupindu umetikisa nchi yetu kwa kiasi kikubwa na kusababisha watu kupoteza uhai na kupunguza nguvu kazi, watoto kuwa yatima wake kwa waumwe kuwa wajane na wengine kuwapoteza ndugu jamaa na marafiki zao.
Siyo mara ya kwanza kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini ila imekuwa ni tabia ya watanzania kuchukulia mazoea na kuuona ugonjwa huu kama michezo ya watoto kwenye televisheni ( TV Game) na huku miaka nenda rudi unazidi kuteketeza watanzania. kwanini watanzania hatulioni hili kuwa ni janga la kitaifa?
Ugonjwa wa kipindupindu ulioanza Agosti 15 2015 katika mkoa wa Dar es salaa na kuenea kwa kasi katika mikoa mingine 20 nchini, kwa mujibu wa taarifa ya tarehe 15 Desemba 2015 kumekuwa na wagonjwa wapya 141 na kufanya jumla ya wagonjwa waliokwa wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma katika mikoa yote iliyoathirika kuwa 184 na vifo vipya viwili.
Tangu ugonjwa huu uanze jumla ya watu 11,257 walipata ugonjwa huu na kati yao 177 wamefariki kwa ugonjwa huu ambayo ni sawa na asilimia 1.5 ya waliougua, mpaka sasa kwa wastani ugonjwa huu umepungua katika mikoa ya Dar es salaamna kwa mkoa wa Iringa na mji wa Moshi kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kudhibiti ugonjwa huu.

Katika tamko la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimua alilolitoa tarehe 16 Desemba 2015 kuhusu mapambano ya ugonjwa wa kipindupindu, Waziri huyo alipiga marufuku uuzaji wa matunda yaliyokatwa na vyakula sehemu za wazi(barabarani) na kutoa amri watakaokiuka wachukuliwe hatua mara moja.
“ Nahitaji nipatate taarifa ya utekelezaji kila siku kutoka kwa Waganga wa Mikoa na Wilaya na Serikali haitasita kuchukua hatua kwa viongozi ambao watashindwa kudhibiti ugonjwa huu katika maeneo yao” alisema Waziri Ummy katika tamko lake kupitia Vyombo vya Habari.
Mara baada ya kutolewa kwa tamko hilo siku tatu baadae mwandishi wa makala hii nilifanya ziara ndogo kuzunguka baadhi ya maeneo ya Jiji la Dares salaam hasa katikati ya Jiji na kugundua kuwa bado kuna uuzaji wa matunda yaliyokatwa na vyakula sehemu za wazi(barabarani) unaendelea. Katika kufatilia hilo kujua nini Jijini limefanya hasa Manispaa ya Ilala ambayo ndo muhusika wa maeneo ya katikati ya Jiji niliwasiliana na msemaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Daud Langa na kutoa ufafanuzi wa suala hilo.
MheshimiwaWaziri wa Afya; Kwaheshimana taadhima kwa position yako naomba nikushauri kuwa sual ahili ni kero kuu kwa Watanzania na hapa hakuna siasa. Mimi kama Mtanzania kwa niaba yangu binafsi na nafsi yangui nataka taka ziondoke mabarabarani. Tena mpeanapo siku hiwe ziondoke leoleo siyo kumwambia mtu mapaka kesho wakati taka zinakaa wiki nzima. Tafadhali Mheshimiwa Waziri kwa kushirikian na vyombo vingine mutuondoshee hii dhihaka ya kupeana masiku wakati Watanzania tunakufa na magonjwa ya aibu. Tumewapa dhamana kwa kuwapa kura na mtuongoze. Kuna vyombo vya uma vya kuzoa taka na kutuondoshea magonjwa. Tulijitokeza kwa kufanya usafi na ni hulka ya Watanzania kuwa wasafi. Tunaambiwaeti tusiende kutupa taka kwanimagari ya kuzoa taka yatapita. Magari hayapitimitaani mpaka mwezi mmoja.Hii si majumngu wala si dhihaka. Maisha ya Watanzania yasifanyiwe dhaihaka tafadhali. Hatuna pakusemea zaidi ya vyombo kama hivi. Rais wetu mpendwa JPM ameowaonesha mfano wa ufuatilaiji nanyi tafadhali tuondosheeni hii adha ya taka na magonjwa. Tafadhali na chonde Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wako. Watanzani tunangoja!!
ReplyDelete