
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana. Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika ukumbi wa mkutano wakati akijiandaa kuhutubia kwenye Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula, kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...