Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Kampuni ya TOSHIBA ya nchini Japan zimetiliana saini Mkataba wa Maelewano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi.
Utiaji saini wa mkataba huo umefanyika Desemba 4, 2015 Jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TGDC ambapo hatua hiyo itaiwezesha TGDC kuweza kupata msaada wa kitaalam ambao utaliwezesha shirika hilo kuweza kuchimba ardhini kwa lengo la kupata mvuke utakaoweza kuzalisha umeme.
Akiongea ofisini kwake, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe amesema kuwa kupitia Serikali ya Japan hususani Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Kampuni ya TOSHIBA watasaidia kuomba ufadhili wa Serikali yao ili kuweza kuendeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na matumizi mengine yanayoendana na nishati hiyo.
“Katika utafiti wa nishati ya jotoardhi tunahitaji watu wenye elimu na uzoefu na ujuzi wa kutosha, miongoni mwa makubaliano ndani ya mkataba huu tuliosaini leo ni wafanyakazi wetu kadhaa kuwapeleka nchini Japan kwenye vyuo vyao ili kuweza kupata mafunzo ya darasani na kutembelea maeneo ambayo Japan wana vituo vya jotoardhi ili wapate ujuzi wa kufanya kazi na Wajapan na kutuletea ujuzi huo hapa nchini”, alisema Njombe.
Aidha, ameeleza kuwa kupitia ushirkiano huo na Serikali ya Awamu ya Tano Japan itaendelea kuisadia Tanzania katika kuendeleza nishati ya jotoardhi kwakuwa ni nishati yenye tija katika kutimiza ndoto za Tanzania kwa kuifanya kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2020.
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi
Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu
toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakiweka saini Mkataba wa wa
Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya
upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es
Salaam.
Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi
Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu
toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakikabidhiana Mkataba wa
Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya
upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es
Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...