Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku
zilizopita.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa
watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa
kila idara za wizara hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu juu
ukaguzi huo katika ofisi za wizara yake ya afya ili kuboresha utendaji
wa wizara hiyo na vituo vyote vya sekta ya afya nchini kote.
Na
Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za
wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao
walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo
mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.
Awali
Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia
ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda
moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda
kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika
wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani.
“Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka
kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla
akiwambia askari wa getini.
Baada
ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa
wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote
ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na
akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda
wa kusaini kuingia umeisha.
Baada
ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa
ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni
jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi
kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini
wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana
wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali
imewaagiza kufanya.
“Nina
wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona
hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa ni kina nani huwa
wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia
watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi
ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya
taifa,” alisema Dkt. Kingwangalla.
Aidha
Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua
ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo
Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi
wanakuwa hawasaini kuwa wametoka.
Pia
alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi
kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole
“Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua
wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi
utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa
kufika na kuwahi kutoka ofisini.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
ReplyDeleteLeo naona wizarani hapa ED kibao zimeletwa na wafanyakazi waliochelewa na kufungiwa nje. Hii ni janja yao. Sasa ED hizi zote zichunguzwe. Madaktari waliotoa hizi ED fake kuwasaidia waalifu kukwepa kuchukuliwa hatua kwa kuchelewa kazini leo nao pia wapewe adhabu kali.
Mdau Alex Bura, Wizara ya Afya
Saa 1.30 ni mapema mno kuripoti kazini. Labda mabachelor ndiyo wanaweza, lakini wale wenye watoto wanaokwenda shule utaratibu huu ni mgumu sana. Mimi naripoti ofisini saa 3.00 natoka saa 12 jioni.
ReplyDeleteIntroduce flexible hours starting 07h30 to 09h00 and finishing between 15h00 and 18h00. Clocking in and out system to be installed. The traffic in Dar is murder and distances cannot be ignored. For your consideration Honorable Minister. I am just being a devil's advocate having same experience in an international organisation out of Tanzania.
ReplyDeleteNi uamuzi mzur kwa mh kigwangala lazima watumishi wafate sheria za kazi
ReplyDeleteNo excuse or any proclastination will be accepted. What labor law is that, anony two and three.
ReplyDeleteIngekuwa saa mbili kamili(8:00 am) asubuhi sawa! lakini saa moja na nusu(7:30 am) sio sawa! huo ni mtizamo tu!
ReplyDeleteHivi huyu mheshimiwa si anakaa kigamboni kwasababu ni mbunge wa kigamboni! wizara ya afya ipo posta na yeye akiwa kama naibu waziri wa afya, aotomatikale atawai kufika ofisini! Anyway ni mtazamo tu!