Elias Maguli Mchezaji wa timu ya Stand United, amekabidhiwa hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/= na wadhamni wakuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara(Vodacom Tanzania) kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi hiyo.
Mchezaji huyo alikabidhiwa hundi hiyo wakati wa mazoezi yaliyokuwa yanafanywa na timu yake katika viwanja vya JKM Park ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga hapo kesho.
Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude(kushoto)akimkabidhi Mchezaji wa Stand United, Elias Maguli(Katikati) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/- kwa kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wa mwezi Oktoba,Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya JKM Park kwa kujiandaa na mchezo wao wa kesho na Yanga,Anayeshuhudia kulia ni Kocha msaidizi wa timu hiyo Athumani Bilal.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Stand United wakiwa katika viwanja vya JKM Park jijini Dar es salaam wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja hivyo kwa kujiandaa na mchezo wao na Yanga wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara hapo kesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...