Mwandishi Wetu

Baada ya kilio cha muda mrefu, hatimaye, wakulima wadogo 21,000 walio katika vikundi 89 vya ushirika katika Kata ya Igomaa, mkoani Iringa keshokutwa wanatarajiwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shbilioni 1 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) nchini kwa ajili ya maendeleo ya shghuli zao za kilimo.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara wa benki hiyo, Robert Pascal alisema maandalizi kwa ajili ya utoaji wa mikopo hiyo yamekamilika.

Wakulima hao wapatewa mikopo hiyo keshokutwa Jumatano (Desemba 30) mwaka huu kijijini kwao Igomaa, baada ya kukamilisha mafunzo na kuandika andiko la mradi na itatolewa kijijini kwa wakulima hao Igomaa lengo likiwa pia kuwachochea wengine kutumia huduma za benki hiyo.

Pascal alisema, mikopo kwa wakulima hao ni mwanzo wa utekelezaji wa malengo ya benki hiyo ambayo si ya kibiashara ya kuwasaidia wakulima waingie katika mnyororo wa thamani wa mazao yao na kufuta dhana kuwa wakulima hawakopesheki.

“Lengo ni kuwawezesha wakulima hao kutoka katika kilimo cha kujikimu hadi cha biashara” alisema na kuongeza kuwa mikopo hiyo kwa sasa imeanza kutolewa kwa wakulima na wengine watafuata katika mikoa mingine mitano.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ukiacha Iringa ni pamoja na Njombe, Pwani, Tanga na Dar es Salaam na mkazo katika mikopo hiyo kwa sasa umewekwa kwa wakulima wa mpunga na mahindi pamoja na wadau wengine muhimu ikiwa ni pamoja na wakulima wa mashamba makubwa.

“Wakulima wa mashamba makubwa pia ni walengwa wetu hususan wale ambao wamekuwa na msaada kwa wakuima wadogo wanaowazunguka” alisema na kuongeza kuwa mikopo hiyo ni ya kwanza toka kuanzishwa kwa benki hiyo ambayo ina mtaji wa zaidi ya sh60 bilioni.

Alisema fedha hizo ni taslimu achilia mbali zaidi ya zingine sh35 bilioni ambazo zipo katika utaratibu mwingine na lengo ni kuhakikisha baada ya miaka itano inakuwa na mtaji wa zaidi ya sh800 bilioni baada na haipo katika kuhudumia wateja wa amana za kila siku kama ilivyo benki zingine.

Alisema mikopo hiyo itatolewa na wakuima watafanya marejesho baada ya kuvuna na wale ambao iatokea bahati mbaya wakaumbwa na majanmga ya binadaamu kama ukame na majanga mengine kuna utaratibu ambao utafuatwa na wataendelea kukopeshwa ili kufidia pengo hilo.

“Tunatoa mikopo ya aina tatu na yote riba yake ni nafuu sana wastani wa tarakimu moja na italipwa kwa awamu na sio wote kwa mkupuo na walengwa kwa sasa ni wakulima wadogo wadogo walio katka vikundi na wanaosaidiwa na wakulima wakubwa” alisema Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa benki hiyo, Francis Assenga.
Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Robert Pascal akizungumza kuhusiana na mikopo kwa wakulima wa kijiji cha Igomaa ambayo itaanza kutolewa keshokutwa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika, jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa benki hiyo, Francis Assenga.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, kuhusiana na mikopo kwa wakulima wa kijiji cha Igomaa ambayo itaanza kutolewa keshokutwa
Ofisa Habari wa Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Saidi Mkabakuli akieleza mzunguko wa thamani kwa wakulima ambao wataanza kukopeshwa na benki hiyo kwa ajili ya kuboresha shughuli zao wakati wa mkutano na wanahabari, jijini Dar es Salam juzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...