Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto for Youth Development Tanzania, Joel Nyakitonto, akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jinsi utengenezaji wa sabuni kutokana mafuta ya mbegu za Mchikichi walipotembelea kiwanda cha Sabuni kilichopo tarafa ya Katubuka ambacho kinamilikiwa na kijana Diocres Dionizi (hayupo pichani) ambaye ni mmoja kati ya vijana 30 aliyenufaika na mafunzo ya Anzisha Biashara Yako (ABIYA) yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa ufadhili wa Shirika la Kazi nchini (ILO).
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakikusanya mbegu kwa ajili ya kukamuliwa kwenye mashine maalum.
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akimtwisha ndoo ya mbegu za Mchikichi zinazokamuliwa na kupatikana mafuta yanayotengenezea sabuni za magadi mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akimsaidia kujaza mbegu za Mchikichi mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo kwa ajili kuzichuja na kupata mafuta yanayotengenezea sabuni za magadi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akivaa koti maalum kwa ajili ya kuingia kiwanda kujionea jinsi kijana huyo anayotengeneza sabuni za magadi zinazotokana mafuta ya mchikichi. Kushoto mmiliki wa kiwanda hicho kijana Diocres Dionizi aliyenufaika na mafunzo ya ABIYA yaliyofadhiliwa na ILO. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...