Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vitakavyotumika kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo.

Msaada wa vitanda kumi utatumika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na wodi nyingine. Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Australia na Tanzania.

Vifaa vingine vilivyotolewa ni pamoja na  Stretcher’  nne zitakazotumika kusafirishia wagonjwa ambao hawawezi kukaa, kifaa cha kufanyia  mazoezi  kwa wagonjwa  na baiskeli ya magurudumu matatu.

 Akipokea msaada huo  Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika hiyo Agness Mtawa ameishukuru Jumuiya hiyo na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kutoa msaada katika hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mseru akizungumza leo katika mkutano uliowajumuisha viongozi wa Jumuiya ya Australia na Tanzania kabla ya hospitali hiyo kukabidhiwa vifaa vya wagonjwa vikiwamo vitanda na baiskeli za magurudumu matatu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mseru leo wakati wa mkutano na viongozi wa jumuiya hiyo na wataalamu wa hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario wa MNH.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi. Agness Mtawa akipokea msaada wa vitanda na vifaa vingine leo kwenye hospitali hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimkabidhi Sister Mtawa vifaa hivyo na kulia ni Mkurugenzi wa jumuiya hiyo, Thierry Murcia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...