Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (Kushoto), akisalimia na Kaimu Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, mara baada ya kuwasili ofisini hapo leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya Naibu Waziri iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini hapo leo asubuhi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Kenan Mhaiki, akijitambulisha wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (hayupo pichani) na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini yake, leo asubuhi. Naibu Waziri Huyo amewasisitiza watendaji wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (Kulia), akiongea na Menenjimenti ya Iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi pamoja na wakuu wa taasisi zilizo chini yake, hapo leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Elias Mshana wakati wa mkutano wake na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi na Wakuu wa taasisi zilizo chini yake , leo asubuhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...