Meli ya Royal iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba, ilipata hitilafu iliyopelekea kuwakawa moto kwa moja ya Injini zake muda mfupi uliopita, kwa Bahati nzuri Meli ya Mv. Serengeti iliyokuwa ikitokea Pemba kwenda unguja ilifika eneo la tukio na kuikuta Meli hiyo na kuanza kutoa msaada wa kuwahamisha abiria waliokuwepo kwenye Meli hiyo na huku shughuli za uzimaji moto na uokozi ikifanyika.Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia tukio hilo na tutaendelea kuwajuza hapa hapa.
Zoezi la Uokozi wa Abiria kutoka kwenye Meli ya Royal na kuingia kwenye Meli ya Mv. Serengeti likiendelea.
Sehemu ya Meli hiyo iliyoshika moto inavyoonekana baada ya Kuzimwa.
Abiria wakihama kutoka kwenye Meli ya Royal na kuingia kwenye Meli ya Mv. Serengeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...