Na Chalilla Kibuda,Globu ya Jamii
WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kuwapeleka
watoto wao kwenye vituo vya afya ili wakapate matone
ya vitamini A na dawa za minyoo ili kujikinga na maradhi
mbalimbali yatokanayo na kukosekana kwa vitamini 'A'.
Wito huo umetolewa Dar es Salaam na Mtaalamu wa
Chakula na Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe
Tanzania (TFNC), Francis Modaha, wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi habari kuhusu uhamasishaji wa
utoaji wa matone ya vitamini A na dawa za minyoo.
Amesema matone ya vitamini
yanatolewa kwa watoto wenye
'A'
umri wa miezi sita na miaka mitano mara mbili kwa mwaka ambapo kwa Tanzania hutolewa mwezi Juni na mwezi Desemba.
Modaha amesema wakati ziezi la utoaji wa matone ya Vitamini A likiendelea kwa awamu ya pili sasa mwezi huu, pia watoto wote wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano hupatiwa dawa ya minyoo.
"Matone ya vitamini A na dawa za minyoo zinatolewa
katika vituo vyote vya afya,ambapo kazi ya utoaji
ilianza Desemba Mosi mwaka huu na itaendelea hadi
mwishoni wa mwezi huu, naomba wazazi walezi kuwapeleka watoto wenu ili wakapate huduma hizo”amesema Modaha.
Modaha, alitoa wito kwa wazazi na walezi kufahamu umuhimu wa vitamini
kwa ukuaji mzuri wa watoto wao kiafya.
'A'
Alitaja baadhi ya sababu za upungufu wa vitamini
'A'
kuwa ni pamoja na ulaji duni usiokidhi mahitaji ya vitamini
'A'
Amesema vitamini
'A'
inahitajika kwa ajili ya ukuaji na
maendeleo mazuri ya mtoto, ikiwa ni pamoja na mifupa na macho.
Aidha amesema upungufu wa vitamini
'A'
unahusishwa na ongezeko vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi, vifo vya watoto, kutoona vizuri katika mwanga hafifu, watoto kuzaliwa kabla ya miezi tisa ya ujauzito na kasi ndogo ya ukuaji na maendeleo ya mtoto na kuongezeka kwa uwezekano wa mtoto kupata maradhi.
Alizitaja njia za kuzuia upungufu wa vitamini
'A'
kuwa ni
pamoja na kuhamasisha unyonyeshaji maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mtoto na kuendelea kumnyonyesha hadi miaka miwili na zaidi..
Alisema kumpa mtoto aliyefikisha umri wa miezi sita vyakula vya ziada ikiwa ni pamoja na vyakula vyenye
vitamini
'A'
kwa wingi pamoja na kutoa nyongeza ya matone kwa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...