Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya ziara katika vituo vya afya vitatu vilivyopo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, yenye lengo la kuzungumza na wananchi wanaopatiwa matibabu kwenye hospitalini hizo na kuwasikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wa kupata huduma.
na kutoa msaada wa mashuka 100.
Akizungumza wakati za ziara hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko huo, Rehani Athuman, alisema kuwa wameamua kufanya ziara hiyo kujua ni namna gani wananchi wanapatiwa kuduma kutoka kwenye vituo hivyo na pia kuwapelekea msaada wa mashuka zaidi ya 100.
Vituo vilivyotembelewa ni pamoja na Mwanerumango, Mzenga na Masaki.
Akiwa katika Vituo hivyo aliwahamasisha watoa huduma kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi lakini pia kuwasilisha madai yao kwa wakati ili walipwe fedha wanazodai kwa Mfuko.
Alisema kuwa suala la uboreshaji wa huduma litafanikiwa tu endapo kila mdau atasimama katika nafasi yake. Alisema kwa sasa ni vyema kila mmoja aka unga juhudi za Rais John Pombe Magufuli ambazo zina nia njema ya kuboresha huduma katika maeneo yote.
Kwa upande wa NHIF alisema kuwa wapo tayari kushirikiana na Wadau wote ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora na hatimaye wananchi kuondokana na kero wanazokumbana nazo kwa sasa.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athuman akizungumza na wananchi juu ya kuwahamasisha watoa huduma kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wanachama wa (NHIF), Katika ziara Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani jana.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athuman akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kituo cha Afya cha Mzenga, kulia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mzinga, Ephrehim Mapunda,wakati wa ziara Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athuman akimjulia hali, Mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kituo hicho, Mauwa Seleman.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...