Mh. Prof. Mbarawa akiongea na menejimenti ya Dawasco na Dawassa kwenye ukumbi wa
Dawasco gerezani,mwishoni mwa wiki jijini Dar.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu
ya jamii) .
Mh. Prof. Makame Mbarawa akisaini
kitabu cha wageni akiwa na Naibu waziri,Injinia Isack Kamwelwe (kushoto), pamoja
na katibu mkuu na naibu katibu mkuu wa wizara ya maji (kulia) katika ofisi ya
afisa mtendaji mkuu wa Dawasco.
Waziri
wa maji mh. Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Dawasco mapema leo alipotembelea makao makuu ya ofisi
hizo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Injinia Cyprian Luhemeja akiwa na waziri wa maji
Prof. Makame Mbarawa mara tu baada ya kuwasili katika ofisi hizo
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco)
limetakiwa kuongeza idadi ya wananchi wanaopata Maji jijini Dar es salaam kutoka
wateja 148,000 waliopo sasa hadi wateja milioni 1 ifikapo Juni 2016.
Akiongea na Menejimenti ya Dawasco na Dawasa ikiwa ni siku
moja tangu kuchaguliwa kwake Waziri wa Maji Mh. Prof Makame Mbarawa alizitaka
Taasisi hizo kuweka mkakati wa lazima utakao hakikisha wateja milioni
wanaunganishwa kwenye mtandao wa Majisafi na salama kwa wakazi wote jijini.
“Tumekuja kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa
bungeni kuhusu Maji. Aliahidi Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine
watahakikisha wana mtua Mama ndoo kichwani” alisema Mh Waziri.
Aliongeza kuwa lazima taasisi hizi mbili zijue wajibu wake
kwa wananchi na kutekeleza ahadi ya Rais ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa
kutafuta Maji na hata wakiyapata gharama zisiwe juu, ameitaka Dawasco
kuhakikisha inawahimiza wateja wake wote na taasisi za serikali kulipia Ankara
za Maji kwa wakati.
Aidha amewahimiza Dawasa kuboresha mtandao wa Majitaka ili
kuwafikia wateja wengi zaidi wanaohitaji huduma hiyo ya Majitaka na kuepusha
usumbufu kwa wananchi unaotokana na Majitaka hayo kuendelea kumwagika ovyo
katika mitaa mingi ya jiji.“Hakikisheni mnaboresha mfumo wote wa Majitaka, uendane na
mahitaji ya sasa ya jiji ili kuwapunguzia wananchi kupata kero mbalimbali
zinazotokana na uchavu wa miundombinu ya Majitaka” alisema Mh.Mbarawa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...