Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na kijana Innocent  Aloyce baada ya kumkabidhi  zawadi ya Toyo, alipomtembelea katika shamba lake
mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita.
 Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel  Raphael (kushoto) akimwangalia  kijana Innocent  Aloyce baada ya kumtembelea katika shamba lake mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni
miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa  “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita.

Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel  Raphael (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na kijana Innocent  Aloyce baada ya kumkabidhi  zawadi ya Toyo, alipomtembelea katika shamba lake
mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita huku akishuhudiwa na ndugu na wafanyakazi
wa Airtel.      



    
Jijini Mwanza  Wilaya ya Misungwi, kampuni ya Airtel kupitia mradi  wake wa *Airtel 
Fursa Tunakuwezesha imefurahishwa na juhudi zilizoonyeshwa na kijana  
Innocent Aloyce mkaazi wa kijiji cha Mwalogwabagole ambaye ameonyesha  
mafanikio katika shughuli zake za ulimaji mbogamboga na nyanya  tangu  
kupatiwa  mashine ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji pamoja na jembe  
la plau miezi mitatu iliopita.

Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, umeendelea
kuwawezesha zaidi vijana  uliowashika mkono,  wanaozidi kuonyesha mafanikio katika kuboresha shughuli zao mbalimbali za kijasiriamali.Ikiwa na lengo la   kuwakwamua vijana kiuchumi na kujiajiri wao wenjewe ili kuondokana na   tatizo la ukosefu wa ajira .



Akielezea changamoto za usafirishaji wa mazao yake  mjasiliamali huyu
ameeleza tofauti anayoiona mara baada ya kukabidhiwa chombo cha
usafirishaji mazao kutoka kampuni ya simu  ya mkononi ya Airtel
walipomtembelea shambani kwake mwishoni mwa wiki hii na kuona maendeleo  yake ya shughuli zake za ulimaji.



Katika kukabidhi pikipiki kwa ajili ya usafirishaji mazao kwa  Innocent,
meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael
amewataka vijana kuiga mfano unaaonyeshwa na Innocent.

Aliongeza kwa kusema “vijana inabidi waachane na dhamira ya kutaka kukaa tu  
vijiweni na kusubiri watafutiwe ajira. Ni juhu di zao wao wenyewe ndio  
zitakazoweza kuwakomboa na kupata maendeleo kama alivyoweza kufanikiwa 
Innocent.

Kufuatia kushikwa kwake mkono na Airtel leo hii  Innocent meweza
kubadilisha maisha yake na familia yake. Hiyo nawahimiza vijana wasikate
tamaa na kujitokeza kwa wingi kwa kuchangamkia fursa hii na nyingine nyingi   
zinazowazunguka”, .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...