Na John Nditi, Morogoro
POLISI mkoani Morogoro imewatia mbaroni watu 23 kati ya hao wawili wakiwa ni wahamiaji haramu raia wa kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kuwa na kibari wala pasi za kusafiria wakiwa njiani kuekelea Afrika Kusini. Raia hao walikamatwa wakiwa Mikumi, wilayani Kilosa.
POLISI mkoani Morogoro imewatia mbaroni watu 23 kati ya hao wawili wakiwa ni wahamiaji haramu raia wa kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kuwa na kibari wala pasi za kusafiria wakiwa njiani kuekelea Afrika Kusini. Raia hao walikamatwa wakiwa Mikumi, wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema hayo Desemba 28, mwaka huu (2015) wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyotokea kuanzia Desemba 20 hadi 27, mwaka huu.
Hivyo alisema , miongoni mwa watanzania waliokamatwa wa nane wanatuhumiwa na kufanya vitendo vya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha katika tukio lililofanyika saa 2: 30 usiku wa Novemba 29, mwaka huu eneo la Lukobe, Manispaa ya Morogoro baaada ya kuvamia Kituo cha wamisionari wanaomiliki shule ya msingi wa hirika la Kidini liitwalo Youth With A Mission.
Kamanda wa Polisi wa mkoa alisema, katika watu hao nane, sita wanadaiwa ndiyo walivamia kituo hicho na kuwapora vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh 3,250,000 pamoja na Bunduki moja aina ya shotgun Pump Action na risasi moja na kutokomea bila kuwajeruhi wamishionari hao.
Kundi hilo la uporaji na ujambazi , 13 kati yao wanatuhimiwa kusafirisha na kuuza dawa za kulevya aina ya bhangi viroba vitatu na maboksi mawili pamoja na misikoto 109 sambamba na dawa inayodhaniwa ni aina ya cocain kete 113.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akionesha sehemu ya madawa ya kulevya yaliyokamatwa
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akiongea na wanahabari
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akionesha pikipiki inayosadikiwa kutumiwa na majambazi
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akionesha gari lililokamatwa na watuhumiwa
Sehemu ya dawa za kulevya aina ya bhangi viroba vitatu na maboksi mawili pamoja na misikoto 109 sambamba na dawa inayodhaniwa ni aina ya cocain kete 113.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...