Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam jioni ya leo December 30, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kumkabidhi  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia.
PICHA NA IKULU














Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi - Ombeni Sefue
  1. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro

  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)

  1. Ofisi ya Makamu wa Rais
            Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
            Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)

  1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)

  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)

  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)

  1.  Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)
Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)
Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Nishati na Madini
Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)
Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Katiba na Sheria
Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)
Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)
Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Mambo ya Ndani
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)
Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)
Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)
James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)
Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
  2. Job D. Masima (Katibu Mkuu 
  3. Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu
Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
30 Desemba, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Eric Shitindi, Kazi na ajira, jembe la ukweli.

    ReplyDelete
  2. Kwa maoni yangu Rais hakuweza bana bajeti kwenye hili. Haina maana kupunguza idadi ya wizara wakati kwenye wizara kuna makatibu wawili au naibu makatibu 2. Hiyo ni sawa na kuwa na wizara nyingine. Sijaona kipya kwenye hili.

    Mdau Mzalendo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inabidi kuelewa mfumo mzima wa uendeshaji wizara ili kutambua ni gharama kiasi gani zimepunguzwa.idadi ya makatibu wakuu sio element pekee ya cost inayoangakiwa.

      Delete
    2. Kaunganisha wizara, ili kupunguza idadi ya wizara, mawaziri na manaibu. Kupunguza makatibu wakuu haiwezekani, kwa sababu ni sawa na kupunguza shughuli za utendaji serikalini.

      Delete
  3. Over 90% ya mawaziri na makatibu wa wizara wamepita shule, vijana wa mashuleni, shule inalipa na siyo bongefReva.

    ReplyDelete
  4. Kazi nzuri sana Rais Magufuli!!!!

    ReplyDelete
  5. Perfect. Asiyeona jipya ame jipanga kutoona jipya!

    ReplyDelete
  6. Kuwa katibu Mkuu shule lazima imekaa HASWA .ila magufuli bwana makatibu wakuu kibao .

    ReplyDelete
  7. Kuwa katibu Mkuu lazima uwe na masters degree na ulikuwa director wa wizara au kampuni Fulani hivi .Mkisikia mtu katibu Mkuu hicho ni cheo cha mwisho serikalini walionakia wote ni wana siasa tu Hapo .mwawaziri manaibu mawaziri wana siasa wengine wameishia high school Mawaziri Kama dyamwale ,Yule MZEE kusanji hawa watu shule no.Makatibu wakuu ndio wezi wenyewe ushawahi sikia katibu Mkuu kafulia kastaafu .wengi wakistaafu makatibu wanapata kazi UN kwenye makampuni binafsi .Mawaziri wakipigwa chini tu wanafulia Hao maana hawana experience ile executive .Mfano mkubwa Sumaye mpaka Harvard kaenda kwa Sababu hajawahi kuwa executive au ukurugenzi au commissioner wa wizara .Ndugu Mkisikia mtu KATIBU MKUU mtu kapiga shule huyo ..

    ReplyDelete
  8. Jamani nae ni binaadamu sio malaika.

    ReplyDelete
  9. Hapa kazi tu. Kwa maslahi ya umma sio binafsi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...