Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly akimkabidhi mkazi wa kijiji cha Kiegea, Bibi Sarah Matereka mbegu za mtama kwa ajili ya shamba lake kama mpango wa wilaya hiyo kuhamasisha wananchi wilayani humo kulima mazao yanayohimili ukame ili kukabili maafa ya njaa , wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofsi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya na katikati ni mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje tarehe 31 Desemba, 2015.
Mmiliki wa shamba la Uzalishaji Mbegu bora za Muhogo aina ya Mumba katika Kijiji cha Choka wilayani Mpwapwa, Edward Kusenha akieleza ubora wa mbegu ya muhogo huo kuwa tangu apande mbegu hiyo mwaka 2014 anaouhakika wa chakula kwa kipindi chote cha hali ya ukame kijijin hapo anayemsikiliza ni Dereva Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu maafa, Nuru Gagu wakati ofisi hiyo ilipokuwa ikifuatilia hali ya upungufu wa chakula kijijini hapo tarehe 31 Desemba, 2015.
Kufuatia ziara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa katika Wilaya za Mpwapwa na Kondoa mkoani Dodoma tarehe 30 Desemba, 2015, iliyolenga kufuatilia hali ya upungufu wa chakula katika wilaya hizo hususan katika maeneo yote yaliyoathirika na ukame. Ofisi ya waziri mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa imetembelea wananchi wa Wilaya hizo na kufanikiwa kuona baadhi yao wanayo mashamba ya mbegu na mazao yanayohimili ukame suala linalowezesha familia zao kuwa na uhakika wa chakula kwa kutohitaji chakula cha msaada kutoka Ofisi ya waziri mkuu.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa inazishauri Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji ambazo ndizo zenye jukumu kubwa la kusimamia masuala ya maafa katika ngazi hizo ziombe mbegu za mazao yenye kuhimili ukame katika Halmashauri zao na kuzigawa bure kwa wananchi badala ya kuwa wanawaombea chakula cha msaada kila mwaka.
Sasa kama njaa imepiga hodi ghafla?? hizo mbegu zitasubiriwa hadi lini zipande na kukua?? watu wafe njaa?.. Kauli zingine wasiwe wanazitoa tu ilimradi siku imepita. Waangalie na hali halisi kwanza suala la mtu kuomba pesa na baadala yake anatakiwa apewe ndoano akavue mwenyewe lisifananishwe na hali kama hii ya njaa! hali hii ni nyingine na ni ya kitofauti kabisa na uhalisia wa jambo!
ReplyDelete