(9/12/2015) siku ya kukumbuka Uhuru wa nchi yetu toka kwa mkoloni wa kingereza, niliamka mapema nikikimbizana ra ratiba na nikiwaza mambo kadhaa. Nilisikitika sana baadaye kugundua kwamba nimewapeleka watoto wangu shule bila kuwaambia kwamba leo ni siku ya uhuru wa nchi yetu. Nimewafundisha watoto wangu mambo mengi kuhusu nchi yetu na nimezoea kuwaeleza kwa undani kuhusu historia yake, viongozi wake, rasilimali zake, vivutio vyake, na uzuri wake.
Nimewafundisha kuiombea Tanzania na viongozi wake kila siku kwa sababu mafanikio ya Tanzania ni mafanikio yao ya leo na siku za mbeleni; na kwamba kwa amani na furaha ya Tanzania nao watakua na amani na furaha. Jioni tulipoketi nao kwa ajili ya chakula nililaazimika kuwaeleza nilichosahau asabuhi. Baada ya kunisikiliza, binti yangu wa miaka 7 aliniuliza ninamaanisha nini kusema “siku ya Uhuru”. Nilichukua muda kidogo kutafuta lugha nyepesi kuwaelezea dhana ya ukoloni na jinsi wazee wetu walivyopambana kutafuta kuwa huru wakiongozwa na akina Mwalimu Nyerere na wenzake.
Nilipofafanua walionesha kunielewa lakini mdogo wake wa kiume akahoji iwapi leo kulikua na gwaride la kijeshi na nikashangaa imekuwaje kwa umri wake wa miaka 6 anafahamu kwamba siku ya uhuru ni ya gwaride. Nikamwelezea kwamba mwaka huu kwa maagizo ya Rais Magufuli, tumeadhimisha siku hii kwa kufanya usafi. Kwa lugha ya kuonesha kutoridhishwa na maelezo yangu, akanijibu kwamba kama imefanyika hivyo sio “fair” maana gwaride ni zuri.
Nilipofafanua sababu za usafi, akaniuliza kwa nini mwaka jana tarehe kama ya leo sikuwaambia kuhusu sherehe za siku ya Uhuru wa nchi yetu. Kabla sijamjibu vizuri, dada yake akarukia tena kukazia kwamba sio mwaka jana tu bali hata mwaka juzi sikufanya hivyo. Mke wangu alipoona nimelemewa akanisaidia kuwajibu kwamba walikua wadogo zaidi na wasingeelewa vema.
Maswali ya watoto wangu yamekua yakizunguka kichwani mwangu na nimejiuliza ni watoto wangapi wakitanzania wa shule za msingi na sekondari wanaelewa maana ya siku ya Uhuru. Watoto na vijana wetu wanaelewa Uhuru huu ni wa aina gani au ni wa kitu gani? Je, wanaelewa nani walituletea uhuru na kwa nini walifanya hivyo? Je, watoto na vijana wetu wanajua nini kilifanyika hadi tukapata uhuru? Je, wanajua majina mangapi ya babu na bibi zao waliotutafutia uhuru? Zaidi ya yote, Uhuru una maana gani kwao leo hii?
Kuendelea kusoma Makala hii bofya hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...