Fredy mgunda ambaye ni chief repoter wa radio nuru fm.
shauri mkwawa a.k.a mama la mama na wafanyakazi wenzake wakifanya usafi.
Wakizungumza wakati wakiwa wanafanya usafi katika eneo hilo wamesema kuwa wameamua kufanya usafi katika hospital hiyo kwa kuwa ndio hospitali inayohudumia wananchi wengi kuliko hospitali nyingine zilizopo mkoani hapa.
Denis nyali ni mhariri wa habari wa radio hiyo amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa lengo la kuwaonyesha wananchi na wafanyakazi wa hospital hiyo kuwa iringa kuwa safi inawezekana kutokana na kauli moja tu aliyoitoa rais imekuwa gumzo kila kona hivyo wananchi wanatakiwa kufanya usafi kila mara na usafi uwe jadi yao.

“Angalia hapa leo hospitali kama hii ya rufaa uchafu wote huu unatoka hapa kama wanagekuwa wanafanya usafi kila siku na kuona usafi ni sehemu ya maisha yao tusingeona hali hii na pia tusinge pata wagonjwa wa magonjwa ya milipuko naomba wananchi wezangu zoezi hili liwe endelevu”alisema denis nyali. 
Hawa muhamed na grace michaeli wamesema ni aibu wananchi kukumbushwa kufanya usafi na rais wakati huo ni wajibu wa kila mwananchi na kuongeza kuwa wanampongeza rais wa awamu ya tano kwa kasi yake anayoendana nayo sasa kwa inawafanya watanzania waanze kuiamini serikali yao tofauti na ilivyo kuwa hapo awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...