Ndugu zangu, Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kupitia kwenu wanahabari ninaomba nitoe salam za mwaka za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Awali ya yote tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametulinda kwa mwaka mzima na kupitia Baraka zake tumeweza kuwa na nguvu, uwezo na hekima za kutimiza majukumu yetu mbalimbali katika kipindi hiki cha mwaka 2015. Tuzidi kumuomba atuvushe salama mwaka 2015.
Ninaomba nichukue fursa hii kuwapongeza Watanzania wenzangu kwa kukamilisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Ninampongeza Mh. Dr John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hongera sana Mama Samia Suluhu kwa kuwa Makamu wa Rais na hongera kwa mwanamichezo mwenzetu Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kushinda ubunge jimbo la Ruangwa na kwa uteuzi wa kuwa Waziri wetu Mkuu.
Hongera za kipekee kwa Mheshimiwa Nape Nnauye kwa uteuzi wa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na hongera pia kwa Mama Anastasia Wambura kwa kuteuliwa kuwa naibu waziri wa wizara hii muhimu kwa mustakabali wa afya na ajira kwa vijana na utangazaji wa jina la Nchi yetu ya Tanzania nje ya mipaka ya nchi. Ninashukuru Mh. Waziri Nnauye majuzi alinipatia fursa ya kuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa vyama vya Kitaifa vya michezo ya kukutana naye na kujitambulisha rasmi kwake, ahsante sana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...