
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba (kulia) leo tarehe 29 Desemba 2015 katika ukumbi wa Selous Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipa majukumu Kamati Maalum ya Wataalam ya kutengeneza andiko maalum litakalotumika kuandaa Programu ya pamoja ya kitaifa ya upandaji miti nchi nzima kuanzia mijini hadi vijijini kwa lengo la kuhifadhi na kuendeleza mazingira ikiwemo misitu. Kwa mujibu wa Prof. Maghembe Kamati hiyo imepewa wiki mbili kukamilisha kazi. Mpango huo utashirikisha pia Wizara ya TAMISEMI.


Duuh naona JM wamekupunguzia kasi. Foreigh Affairs ndio ingekufaa ujinoe ila sasa naona unapata uzoefu wa kupanda miti.
ReplyDeleteKwa maoni yangu mazingira tuyajuayo sisi ni pamoja na mitaa tunayoishi sisi wananchi wakawaida. Tafadhalini wadau na watoa maamuzi mtusikilize sisi wananchi wa kawaida tunakerwa na maji taka yanayochafua mazingira. Hebu tafadhalini waheshimiwa wote haya mazingira yetu yenue Waziri special tuangalizieni na mutusafishie. tuko tayari kuendeleza usafi na infrastructure mtakazotuwekea. Mumejenga mitaro yamajitaka, haifanyi kazi inatirirsha majimachafu mabarabarani.Tafadhalini watoto wetu nasi wenyewe tunatembea kwenye vinyesi na uchafu. Ni aibu yetu sisi wenyewe. Magari ya taka hayapiti mitaani na taka simetujaalia huku manyumbani mwetu. Tafadhali Waziri wa Mazingira na Waziri unayehusika na Mitaa kuweni serious. Nyinyi mmesafika na kuzungumzia mazingira ya miti na misitu,TUTAZAMIENI MITAA YETU. Hata hilinalotumngojee Mheshimiwa rais aseme au amfukuze mtu kazi? Tafadhalini jamani.
ReplyDelete