Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akitembelea maeneo mbalimbali ya Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza na Watendaji na baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini.
“Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu” Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali.
Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.
This is dumb and most stupid idea. Wakati ambapo bado serikali haijaanzisha mtanda wake pekee unaoptikana kila mahali itakuwa ni kisingizio kwa wengine kwamba hawakuwa na mtando wenye uwezo wa kufungua mtanda wa serikali kwa ajili ya kupata taarifa ama nyaraka. First things frist. Serikali ijenge mtandao wenye kuaminika sasa hivi hata hapa Dar es salaam ni vigumu kufungua gov. tz network!
ReplyDeleteAnony wa kwanza hapo juu, sitakuwa nimekosea nikisema kwamba una jazba. Vile vile mtu yeyote akisoma uliyoyaandika hapo juu hasa sentensi yako ya kwanza ataona vivyo hivyo, japo sio lazima kusema, lakini mimi nimeonelea niseme machache.
ReplyDeleteBelieve me, jazba is an attribute or good indicator of dumbness and stupidity.
Aliyoyasema kiongozi ni maagizo na sio sheria,lakini hata kama ni sheria na ikabainika kuwa isiyo na tija au isiyotupeleka mbele, basi itarudishwa mjengoni ki-utaratibu ili ifanyiwe marekebisho. Mimi sijawahi kufanya kazi serikarini wala sitegemei, lakini kwa kuangalia, kusikiliza na kujifunza kwangu ki-binafsi naelewa kwa kiwango hicho. Vinginevyo unisaidie wewe na nitashukuru. Anony nakuomba jiulize swali hili. Je, kama wadhifa huo angepewa mwenye jazba maamuzi yake yangekuwaje?
Anony tayari umekwisha kutoa elimu kwa watumishi kuwa watatoa KISINGIZIO kwamba hawakuwa na mtandao wa kufunguwa b/pepe za kiserikali. Kisingizio!? (proclastination, excuses)Awamu ya tano haina nafasi ya watumishi kama hao. Je, na wewe umejipanga kujipanga kutoona JIPYA? pole sana. Adija aliselema!! Adija aliselema, selema, selema.... Anony uko nje au ndani ya nchi? Hii ni Tanzania mpya.
"HAPA KAZI TU"
MbitiNgosha.
Ngosha tetea wakwako tu lakini ukweli ni kwamba hata kama annony ana jazba kama unavyodai ukweli upo wazi kwa wengi. Mtandao wa Serikali bado unamapungufu mengi sana nanunataka kufanyiwa kazi zaidi. Sasa kazi tu bila mfumo unaowezesha kazi kufanywa? Nakubaliana nawe stupid it is not. Lakini mapungufu hayo hayatawezesha kufanikiwa kwa lengo linalokusudiwa hata kama limetoka mbinguni.
ReplyDelete