Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
Wanafunzi wa Madrasa mbali mbali za Zanzibar wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...