Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho
la Vyama Watu wenye Ulemavu Tanzania(SHIVYSWATA) Amon Anastaz Mpanju
akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpongeza Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa kutimiza ahadi
yake ya kuyajali na kuyapa kipaumbele
masuala ya watanzania wenye ulemavu kwa uteuzi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi Vijana na Ajira Dk.Abdallah Possy, kulia ni Mwekahazina Alias
Masamaki
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la Vyama Watu wenye Ulemavu
Tanzania(SHIVYSWATA) Amon Anastaz Mpanju.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu
ya jamii).
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Vyama vya Watu Wenye
Ulemavu (Shivyawata), limesema kuwa changamoto zinazowakabili watu wenye
ulemavu nchini ni ukosefu wa mazingira rafiki
ya kupatia elimu kwa jamii hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Shivyawata , Amon Mpanju amesema kuwa kwa
serikali ya awamu ya tano iweke mkazo katika mazingira ya watu wenye ulemavu
ikiwemo na upataji wa habari kwa kundi la watu wasiosikia.
Mpanju amesema kuwa watu wenye
ulemavu wamekuwa na sera lakini hajawahi kutekelezwa katika serikali zilizopita
hivyo kwa serikali ya awamu ya tano
itekeleze sera kwa vitendo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...