Familia ya marehemu Mwalimu Ngore N. Kondo wa Chang’ombe, Dar es salaam tunapenda kutoa shukrani zetu
za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nasi kwa kutufariji kwa hali na mali katika
kumuuguza mpaka kumzika baba yetu mpendwa aliyefariki tarehe Novemba 28, 2015 katika hospitali ya Regency na
kuzikwa tarehe Novemba 29, huko Chamazi.
Shukrani za pekee ziwafikie Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa hospitali za Hindu Mandal na
Regency za hapa DSM. Pia shukrani ziwafikie Uongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Watumishi wa Umma
(Magogoni) ambapo marehemu alifanya nao kazi kwa zaidi ya miaka thelathini (30). Na pia shukrani
ziwafikie Uongozi na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania, Hospitali ya Aga Khan pamoja na Kinondoni
'B' Dispensany & Medical consultant na Benki ya NMB ambako watoto wa marehemu Hadija, Nasra na
Abdul ni watumishi wa taasisi hizo.
Ni vigumu kuwashukuru wote kwa majina. Tunawashukuru wote, ndugu, jamaa, marafiki na majirani wa
Chang’ombe na Chamazi kwa ushirikiano wenu mkubwa.
Tunapenda pia kutumia nafasi hii kuwataarifu na kuwakaribisha katika shughuli ya arobaini na hitma ya
marehemu baba yetu mpendwa itakayofanyika Jumapili ya tarehe 3 Januari, 2016 saa sita mchana
nyumbani Chang’ombe.
Inna Lillahi wa inna ilayhi Rajiun
“Hakika, sisi ni wa mwenyezi mungu
na hakika kwake tutarejea” –
Quran 2:156
Mwalimu wetu masikini, pole Hadija, pole wote
ReplyDeleteTupo pamoja Kapilino na Nasra.Apumzike mahala pema
ReplyDeleteInna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiun, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema pepon Amen.
ReplyDeletepoleni wanafamilia hakika pengo lake kuzibika ni vigumu innalilahi wainnailahi rajiun pumzika kwa amani mwalimu wa mikato Mr. Kondo
ReplyDelete