WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu. 
 Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini Dodoma. 
 Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu wa siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa. “Hadi ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia unapoondolewa huo kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika wa hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka”alisema Simbachawene. 
 Aidha aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya haitaendelea kuwalea watendaji wavivu.
 Kwa upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.
 WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
 Naibu waziri  nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora, Selemani Jaffo akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
 wafanyakazi wa wizara ya ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora wakimsikiliza waziri wao  George Simbachawene.

 WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...