Na Bashir Yakub
Makosa ya jinai ni makosa yote yaliyoorodheshwa katika sura ya 16 ya kanuni za adhabu pamoja na yale yaliyo katika sheria nyingine kama ile ya uhujumu uchumi. Pamoja na kuwapo sheria nyingine ambazo huorodhesha makosa ya jinai bado Kanuni za adhabu inabaki kuwa sheria kuu inayoorodhesha makosa ya jinai. Kwa ujumla katika sheria tunayo makosa makuu ya aina mbili.
Kwanza ni hayo ya jinai na pili ni ya madai. Kwa kusema makosa ya jinai na madai unajikuta umeongelea karibia makosa yote unayoyajua na usiyoyajua. Kila kosa unalolijua kichwani mwako lipo katika moja ya makundi haya.
Kwa mifano tu makosa ya jinai ni kama kupiga, kutukana, kuendesha kwa uzembe( ulevi, kuongea na simu, mwendo kasi,kuzidisha abiria n.k), kudhalilisha, kuiba, kubaka, kuua, utapeli, kughushi, ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya ofisi ya umma, kulawiti, kumiliki madanguro, ukahaba, dawa za kulevya( kutumia au kuzimiliki), kuzuia mahakama au mamlaka za kisheria kutekeleza wajibu, kuharibu mali ya mtu, kuvamia eneo la mtu kwa nia ovu, manyanyaso ya jinsia na mengine mengi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...