Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Initiative for Policy & Education(UIPE), Isack Dornad akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya waandishi wa  habari wakimsikiliza 
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Initiative for Policy & Education(UIPE), Isack Dornad  jijini Dar es Salaam leo. 
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Zainabu Hamis, Globu ya Jamii
TANZANIA ni miongoni mwa nchi 100 Duniani zilizo huru Kiuchumi, pia imeshika nafasi ya 82 ya Uhuru wa Kiuchumi Dunia kwa mwaka huu.

 Nafasi hiyo ime
tolewa na Umoja wa Shirika lisilo la Kiserikali lijulikanao kama Mtandao wa Uhuru wa Kiuchumi kutoka nchini Canada.

Akizungumza na waandishi wa habari jijijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Initiative for Policy & Education(UIPE), Isack Dornad amesema kuwa,Tanzania imepanda nafasi kumi katika ripoti ya mwaka huu kutoka nafasi ya 92 katika ripoti ya 2014 hadi kushika nafasi ya 82 katika ripoti ya 2015 na kushika nafasi ya tatu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amezitaja nchi mbalimbali zilizoongoza katika nafasi 10 bora ambazo ni Hong Kong, Singapore, New Zealand, Switzerland, United Arab Emirates, Mauritius, Jordan, Ireland, Canada, Uingereza na Chile.

 Pia amezitaja nchi zilizo shika mkia kuwa ni nchi ya Angola, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Zimbabwe, Algeria, Argentina, Syria, Chad, Libya, Jamuhuri ya Kongo na Venezuela.

Aidha Dornad ametaja vikwazo mbalimbali vinavyo sababisha Tanzania kuwa nyuma kiuhuru wa uchumi kuwa ni pamoja na Ulazimishwajia wa kuchangia huduma za kiserikali, Mikataba ya Ajira Kima cha chini cha Mishahara, Kumiliki akaunti za benki za fedha za nje, Viwango vya juu kwenye kodi za mishahara na vipato, malipo ya ziada, hongo na upendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Angola (almasi,mafuta), Libya (mafuta), Venezuela (mafuta), Congo (almasi, urani) - utajiri wote huo wa hizo rasilimali halafu zimeshika mkia, laa haulaa, kumbe rasilimali hazisaidii sana kama uongozi wa taifa haujui kuzitumia kwa maslahi ya wananchi.

    ReplyDelete
  2. Lipi jema linalotoka Zimbabwe nowadays? Kila ukichungulia news ni majanga tu..

    ReplyDelete
  3. Hawa waandaaji wa report hii wangebainisha sababu za msingi zinazofanya nchi nyingi za afrika kudolola kiuchumi. Kwa mfano, ingekuwa vema kama wangebainisha kuwa viongozi wengi wa Afrika (ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari) ndio wanaosaidia nchi za kibepari kuiba mali za Afrika (copper,diamond,gold,oil nk) na kuwanufaisha wao (imperialists, multinational corporations, and African puppet leaders) na kuacha uchumi wa nchi hizi zikididimia kiuchumi na wananchi wake walio wengi kuteseka bila sababu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...