Kampuni ya TCCIA Investment Limited imeongeza mtaji wake kutoka Tshs Bilioni 21 mwaka 2013/2014 hadi kufikia Tshs Bilioni 33 mwaka 2014/2015 kutoka kwa wanahisa wake. 
 Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa kumi wa wanahisa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori alisema ongezeko hilo linatokana na usimamizi mzuri wa Bodi ya wakurugenzi wa TCCIA Investment Company Limited, kufanya kazi kwa ufasini na waledi.
 “Miaka kumi iliyopita mtaji wetu ulikua ni kiasi cha Tshs bilioni 2 lakini kwa sasa tunaongelea bilioni 33 kuishia Desemba mwaka 2014,” alisema Kamori. 
 “Sisi ni wadogo, lakini tunakwenda vizuri, hii inatokana na usimamizi mzuri wa watu wetu wa mahesabu kwa kushirikiana na Bodi,” aliongeza. 
 Alisema mwaka 2014 kampuni ilipata faida ya jumla ya Tshs Milioni 784 Kabla ya kulipa kodi ambayo aliielezea kuwa ongezeko kubwa kulinganisha na mwaka 2013 ambapo faida ilikua ni Tshs milioni 588. 
 Kutokana na kupata faida kubwa, kampuni imeridhia kutoa gawio kwa wanahisa wake ambapo itatumika jumla ya Tshs milioni 274. 
 “Kutokana na hilo Bodi imeridhia kulipa gawio la Tshs 48 na senti 26 kwa kila hisa moja kwa mahesabu yaliyokaguliwa ya mwaka 2014 kulinganisha na gawio la Tshs 36 na senti 96 kwa mwaka 2013 kwa hisa moja,” aliongeza. 
 Akizungumzia mwenendo wa kampuni na ukuaji wake, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Mhandisi Aloyce Mwamanga, alisema kwa sasa kampuni ipo katika mchakato wa kubadilisha jina kutoka TCCIA Investment Company Limited na kuwa TCCIA Investment Public Limited Company. “Kutokana na sheria ya makampuni ya mwaka 2002 kampuni ikishazidi wanachama zaidi ya hamsini ni lazima ijulikane kama ni public na sio binafsi,” alisema Mwamanga. 
 Aidha aliwataka wanachama kuzidi kuwekeza katika kampuni hiyo kutokana na kukua kwa kampuni yao kila mwaka.
 “Kampuni yetu inakua kila mwaka, hivyo ni fursa ya wanahisa hasa wale wadogo kuwekeza,” alisema. Aliongeza kuwa ifike mahali wanachama wenyewe wawe ndio wamiliki wa kampuni kwa asilimia kubwa na kusema kuwa uwekezaji ni jambo zuri.
 Wajumbe wa mkutano Mkuu wa kumi wa wanahisa wa Kampuni ya TCCIA Investment Limited wakisikiliza moja ya mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanahisa hao kabla ya kuanza mkutano huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Kampuni ya TCCIA Investment Limited, wakimsikiliza mtoa mada, Bw. Arphaxad Masambu, kwenye smina ya kuwajengea uwezo kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa muda wa Mkutano Mkuu wa wanahisa wa TCCIA Investment Company Limited, Mhandisi Peter Chisawilo (kushoto) akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa kampuni hiyo (hawapo pichani) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...