Mkali wa magoma hapa nchini na nje, Dj Bon Love akifanya yake katika Usiku wa Heart & Soul uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota kinachobamba zaidi hapa mjini cha Raphsody, ndani ya Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar. Dj Bon Love na maDJ wengine wakali hukutana pamoja kwenye kiota hicho ili kukonga nyoyo za wapenda Burudani kutoka maeneo mbalimbali.Usiku huo uliwezeswa kwa Udhanimi Mkubwa wa Kilaji ya Heineken.
Baadhi ya Wadua wa Burudani wakiwepo DJ. Venture na Mwanalibeneke Haki Ngowi wakiwakilisha katika Usiku wa Heart & Soul.

Mmoja wa maDJ wanaopiga katika Usiku wa Heart & Soul akifanya mambo yake.
![]() |
Dj Bonny Luv na mdau |
Mdau Othman Michuzi (kulia) na marafiki wengine nao hawakutaka kupitwa Usiku wa Heart & Soul ndani ya kiota pendwa cha Raphsody, Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...