Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD). 

Na Rabi Hume.

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez amezitaka serikali za nchi za Afrika ikiwemo serikali ya Tanzania kutekeleza vyema sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kuhuisha sera ya viwanda kwa ajili ya mipango ya ukuzaji wa viwanda.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD). Shughuli iliyofanyika Chuo cha Diplomasia cha Msumbiji na Tanzania, kilichopo Kurasini Dar es salaam.

Katika hotuba yake hiyo alisema suala la Sera za ubunifu ni mpya kwa mataifa mengi ya Kiafrika na hivyo hazitekelezwi vyema na kusema pia mifumo ya uvumbuzi inakabiliwa na changamoto nyingi.

Alisema sera nyingi za viwanda katika nchi za Afrika hazikujenga mfumo wenye kuchagia mafunzo ya teknolojia na utekelezaji wake.
 
Naibu Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Bw. Bernard Achiula akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa UN nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).

“Na hata kama kuna sera za maendeleo ya viwanda sera hiyo haikuratibiwa vizuri na suala la sayansi teknolojia na uvumbuzi.” Alisema.

Alisema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuhakikisha kwamba zinaoanisha yote hayo ilikuwa na sera madhubuti ya mazingira yenye lengo la kuendeleza viwanda, teknolojia na sayansi vikiwa pamoja.

Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Mataifa (UN) kuzindua ripoti inayohusu Teknolojia na Ubunifu duniani 2015 jijini Geneva, Switzerland, ofisi ya UN Tanzania imezindua ripoti hiyo nchini na kuonyesha hali iliyopo Afrika.

Dkt. Bitrina Diyamett kutoea Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STIPRO), akidadavua ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa ripoti hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...