Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli alitoa agizo la kumtaka kila mtu kuadhimisha siku ya
kumbukumbu ya Uhuru tarehe 9 Disemba, 2015 kwa kushiriki zoezi la kufanya usafi
wa mazingira.
Katika Mkoa wa Dodoma, zoezi hilo litahusisha
kazi za usafi wa makazi na maeneo ya shughuli mbalimbali, kufagia barabara za
lami na vumbi, kufyeka nyasi kandokando mwa barabara na katika maeneo ya wazi
na jamii, kuokota takataka (mifuko ya Rambo) na kuzibua mitaro ya maji
ya mvua kama ipo katika eneo husika
kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa
kupitia Ofisi zao ndio waratibu wa zoezi la usafi kwenye Wilaya husika. Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, ameainisha maeneo ambayo taasisi
mbalimbali za Mkoa wa Dodoma zitayashughulikia kufanya usafi Mjini Dodoma (Orodha
imeambatishwa).
Kutokana na uhaba wa vifaa vya kufanyia Usafi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma anashauri taasisi mbalimbali zitakazohusika na
zoezi la usafi wa mazingira, ziwe na vifaa vyake vya kufanyia usafi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma anasisitiza
zoezi la usafi kwa taasisi, lizingatie maeneo yaliyotajwa kwenye jedwali lililoambatishwa na Uongozi wa
Serikali Mkoa wa Dodoma unamtaka kila mwananchi na taasisi zilizopo Dodoma
kushiriki kikamilifu katika usafi huu.
Imetolewa na:
OFISI YA
MKUU WA MKOA
DODOMA
Disemba 8,
2015



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...