Picha ya Meli MV-Mapinduzi II ilipokuwa katika hatua za matengenezo Nchini Korea Kusini
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)akikata utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa Meli ya MV-Mapinduzi II katika bandari ya Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar akiwepo na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kulia) Nahodha wa Meli hiyo Abubakar Mzee (kulia) na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mabaharia waMeli ya MV-Mapinduzi II baada ya uzinduzi rasmi uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar,pamoja na kuitembelea kukagua sehemu mbali mbali za meli hiyo akiwa na Viongozi mbali mbali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na wafanyakazi wa Kike katika  Meli ya MV-Mapinduzi II wakati alipokuwa akifanya ukaguzi na kutembelea sehemu mbali mbali za Meli hiyo akiwa na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao baada ya uzinduzi rasmi  uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakipata maelezo kutoka kwa Nahodha wa Meli ya MV-Mapinduzi II Abubakar Mzee (katikati) wakati walipofika katika chumba maalum cha mitambo ya kuendeshea meli inapokuwa safarini,maelezo hayo yalitolewa katika shamra shamra za sherehe za uzinduzi uliofanyika leo katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...