Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha  Wizarani kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 12 Desemba, 2015. Aliyesimama pembeni ni Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo.
Mhe. Balozi Mahiga akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mhe. Balozi Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Nsia Paul wakati wa mapokezi yake Wizarani
Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Suzan Kolimba akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Tagie Mwakawago mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimpokea Mhe. Waziri Wizarani. Pichani Mhe. Waziri akisalimiana na Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora. Kwa picha zidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...