KAMPUNI ya Msama Promotions ambayo ni waandaaji wa Matamasha ya Pasaka na Krismasi, imetangaza viingilio vya juu kwenye Tamasha la Krismasi kuwa ni Shilingi 50,000 kwa viti maalum, Tamasha ambalo litafanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linalokwenda na shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 ambako kabla, Msama waliandaa tamasha la Kuombea Amani uchaguzi Mkuu lililofanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama VIP watachangia shilingi 10,000 na viti vya kawaida watachangia shilingi 5000.Msama alisema watoto watakaohudhuria tamasha hilo watachangia shilingi 2000, alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo lina lengo la kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

"Watanzania tujitokeze kwa wingi ili turudishe shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa tofauti na chaguzi zilizopita, hivyo ni nafasi yetu kumwambia Mungu asante baada ya kutupitisha katika tukio hilo muhimu," alisema Msama.

Aidha Msama michango inayopatikana kupitia viingilio hivyo hurudisha kwa Jamii yenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na wengineo wenye uhitaji kama huo.Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanakwenda vizuri, huku waimbaji kama Rose Muhando, Upendo Nkone, Ephraim Sekeleti, Rebecca Malope, Kwaya ya Wakorintho Wapili, Joshua Mlelwa na Christina Shusho wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...