Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kifurushi nafuu cha ‘Yatosha Intaneti’ na ubia kati ya kampuni hiyo na Google ambapo mteja wa Airtel ataweza kupata huduma ya kutazama video zilizopo You Tube Bure. Kulia ni Meneja wa Huduma za Intaneti wa Airtel, Erick Mshana.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) na Meneja wa Huduma za Intaneti wa Airtel, Erick Mshana wakizindua kifurushi nafuu cha ‘Yatosha Intaneti’ na ubia kati ya kampuni hiyo na Google ambapo mteja wa Airtel ataweza kupata huduma ya kutazama video zilizopo You Tube Bure katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
· Airtel waingia ubia na Google kuwezesha wateja kucheki video BURE
· Bure kupitia vifurushi vya Yatosha intaneti
KAMPUNI inayoongoza katika mtandao wa intaneti Tanzania, Airtel leo imeungana na Google katika kuwapatia wateja huduma yakutazama video mbalimbali zikiwemo zile za kiswahili BURE kupitia You Tube mara tu wanapojiunga na vifurushi vya Yatosha intaneti.
Airtel imetangaza kuwapatia wateja wake ofa hiyo ya kuona video za You Tube BURE mara baada kuzindua kifurushi nafuu cha YATOSHA INTANET, Airtel imeeleza kuwa huduma hiyo ya BURE ni muendelezo wa dhamira yao ya kutoa huduma bora za intaneti kwa wateja wake zaidi ya milioni 10 nchini Tanzania ambapo wateja wa Airtel watakaojiunga na YATOSHA INTANET sasa wataweza kujipatia maudhui ya video nzuri wapendazo bila kufikiria tena gharama.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa huduma za inteneti wa Airtel Tanzania Gaurav Dhingra, alisema, "dhamira yetu siku zote ni kuendelea kuwa karibu na wateja wetu, kuelewa mahitaji yao na kuweza kuwapatia huduma bora yenye viwango vinavyohitajika.”
“Tunafahamu vizuri kwamba wimbi la uhitaji wa huduma hii ni kubwa kwa sasa, ongezeko la wanaokupakua au kuona video za aina mbali mbali zikiwemo michezo, muziki, habari za aina mbalimbali kupitia You Tube imeongezeka kwa kasi sana kutokana na wateja wetu wanavyoridhishwa na huduma zetu bora za intaneti.” Alieleza Dhingra
Bw Dhingra akiendelea kufafanua alisema “Hata hivyo, watumiaji wa huduma hiyo ya kutazama au kupakua video hizo bado wamekuwa na kikwazo cha kufikiria swala la gharama na kutofurahia ubora wa video hizo, hivyo basi Airtel tumeamua kuwapatia wateja wetu MB’s za BURE kupitia You Tube ili waweze kufurahia kuangalia Video kupitia intaneti ya Airtel ".
Charles Murito, Meneja mwakilishi wa google nchini Tanzania, alisema ; "Tunataka kuhakikisha kwamba watumiaji wa simu za mkononi wanaongezeili na kufurahia huduma za You Tube nchini. Kwa kushirikiana na Airtel tutahakikisha kwamba wateja wote wa simu za mkononi wanaweza kutumia simu zao kwa kuangalia video kwa urahisi zaidi na kwa gharama nafuu wakiwa mahali popote. Vile vile watafurahia kutumia You Tube ikiwa na maudhui ya lugha ya Kiswahili na kuweza kufurahia mambo mbalimbali kwenye muziki, habari za biashara, burudani na elimu " .
Akielezea jinsi ya mteja kuweza kujiunga na vifurushi hivyo, Afisa huduma za intaneti wa Airtel Tanzania Erick Daniel Mshana, alisema “mteja wa Airtel wa malipo ya awali anaweza kupata huduma hii kwa kupiga *149*99# kisha kujiunga na kifurushi cha Yatosha intaneti na atafurahia huduma yetu ya Intaneti aliyojiunganayo ikiwa ni ya SIKU, WIKI, au MWEZI na zaidi ataona video za You Tube BURE.
Airtel pia tuwakaribisha wadau mbalimbali wanaotengeneza na kusambaza video kwa njia ya mtandao kushirikiana nasi kufikisha video zako kwa jamii kupitia OFA hii. Kama wewe ni mtoa huduma wa video, unaweza kuwasiliana nasi kupitia Airtel huduma kwa wateja".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...