.Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufugaji wa sungura unaweza ukawasaidia wakulima katika kujiongezea kipato kwa mbali na kuuza nyama yake lakini pia wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake,katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson, akiwaonesha waandishi moja ya sungura wanaopatikana katika shamba hilo, kulia ni Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange, katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
 Sehemu ya mabanda ya kufugia Sungura hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba akifafanu jambo kwa Wandishi wa habari  katika ziara ya mafunzo  kuhusu mradi  huo  katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
 Picha na Emmanuel Massaka waGlobu ya jamii


WATANZANIA wameshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura ili waweze kujiongezea kipato kutokana na mnyama huyo kuwa na faida nyingi.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo jana katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoani Pwani.

Dickson alisema, ufugaji wa sungura unaweza utawanufaisha wakulima katika kujiongezea kipato  mbali na kuuza nyama yake wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake

“Tunawafundisha wakulima jinsi ya kufuga sungura ili waweze kunufaika, lakini wanaweza kujiuliza ni wapi wanaweza kuwauza wakishafikia hatua ya kuuzwa, sisi tunawapa soko kwa hiyo kikubwa kwa mkulima ni kufuga tu,” Dickson alisema.

Alisema kampuni yake ina mashamba ya sungura hivyo wanapoingia mkataba na wakulima wanaohitaji kufuga wanakubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuwatafutia masoko ambapo wao wenyewe wananunua sungura hao. 

Alisema mbali na faida ya kuuza nyama yake lakini pia wanaweza kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake.                                                                                  

Naye Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange alisema, kuna umuhimu wa kinamama  kutumia fursa ya ufugaji sungura ili kumudu kuwasomesha watoto wao badala ya kuwategemea waume zao.

Alisema licha ya kuwa sungura hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kuwafuga lakini amekuwa akihakikisha kuwa waishi katika mazingira mazuri ili waweze kumpa faida.

“Huu ufugaji kwa kuwa ni mpya watu, wengi wanaweza kujiuliza inakuwaje au masoko watapata wapi...lakini mimi nilipoanza kufuga niliingia mkataba na hii kampuni na wao walinipa masoko ina maana kwa kila sungura wa kilo nne nauza kwa Sh 40,000,” Nyange alisema.

Nyange alishauri wajasiriamali na hasa wanawake kujiingiza katika ufugaji huo ili waweze kufanya mambo yao mbalimbali bila kuwategemea akinababa ambao wakati mwingine wanakuwa na majukumu memgi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. duh sijawahi kusikia watu kula nyama ya sungura , najua watu hufuga sungura kama vile watu wanavyofuga kasuku au mbwa au paka , hii ya kufuga kwa ajili ya kumla nyama yake naona mpya , naomba kuelimishwa

    ReplyDelete
  2. mr.Anonym hapo juu, kwani sungura anatofauti gani na kuku anayefugwa na mwishowe kuchinjwa ili aliwe? unapokula nyama ya kuku toka maduka ya chakula wallmart au supermarket unafikiri wamemtoa wapi?

    ReplyDelete
  3. mimi pia nimfugaji wa sungura ninao wengi lakini tatizo soko akuna naomb kampuni ii ije na kwe2 songea

    ReplyDelete
  4. Nitapata mbegu ninaitaji sungura 0763370175

    ReplyDelete
  5. Nahitaji mbegu 0655310987

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2016

    naomba namba ya huyo mama ili niweze kuwasiliana naye. maana nataka nianzishe mradi huo. ninamalizia ujenzi wa halls kwa ajili ya kazi hii.

    ReplyDelete
  7. Naomba mawasiliano yenu ili nipate kuja kuwatembelea nahitaji kufuga.

    ReplyDelete
  8. Naomba nmba ya yenu ilinipate

    ReplyDelete
  9. Naomba nipatie mawasiliano ya DILA Afrika au ofisi zao zilipo niwatembelee kwa ushauri zaidi wa mradi wa sungura hakika nimeupenda.

    ReplyDelete
  10. Habari wadau Sungura hawa anaenunua nani? atupe number yake tumtafute bs

    ReplyDelete
  11. Habari wadau Sungura hawa anaenunua nani? atupe number yake tumtafute bs

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...