Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba akizungumza na waandishi habari juu ya mikakati mbalimbali ya uzalishaji umeme katika mazungumzo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji na Huduma kwa Mteja), Mhandisi Sophia Mgonja, Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir Kachwamba, kushoto kutoka kulia ni Meneja Uhusiano Adrian Severine.
Waandishi habari wakimisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felschimi Mramba leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limewafukuzisha kazi watumishi waandamizi wa Tanesco upande wa maneja na wahasibu kutokana na ubadhirifu wa fedha katika utumishi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba amesema kuwa shirika halitaweza kuwaacha watendaji wakawa wanafanya kazi kwa rushwa wakati wanalipwa mishahara.

Amesema wataendelea kuchukua hatua kwa watendaji wote watakabainika kufanya udanganyifu au kutoa lugha zisifaa kwa wateja na wakati mwingine kuomba fedha kwa huduma ambazo ni haki ya mwananchi kupata.

Mramba amesema Tanesco imeongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi megawati 300  sawa na asilimia 115  na kufanya kuwa na umeme wa uhakika huku miradi mingi ikiendelea kufanyika.

Amesema  wanatarajia kupata megawati 240 kutoka Kinyerezi namba mbili  wakati wowote  na kufanya shirika kuwa na umeme wa uhakika.

Aidha amesema wakati wa suala miundombinu likifanyiwa kazi wananchi wawe wavumilivu wa kukatika umeme katokana na kuboresha miundombinu hiyo.

Aliongeza kuwa wanaotaka kufanya kazi na Tanesco kwa kupata nguzo lazima wazalishe nguzo zenye ubora wa kuweza kuhimili kwa muda mrefu bila kuanguka kuanguka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Majizi yameiba na kudhulumu nchi kwa miaka. Mimi si mtu mwenye wivu,au kisasi I think, lakini kuwaonea hawa watu huruma na kuwafukuza kazi tu naona haitoshi. Tujenge jela nyingine ikiwa kuna upungufu wa prison cells.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...