Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) wakati alipokitembelea kituo hicho cha Polisi jijini Dar es Salaam leo. Pia Waziri Kitwanga katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza wizara hiyo, alitembelea Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), pamoja na kukagua nyumba za Makazi ya Polisi za sasa na zamani zilizopo barabara ya Kilwa. Wanne kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akitoka kuikagua moja ya nyumba ya zamani ya Jeshi ya Polisi ambayo inakaliwa na baadhi ya askari iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Waziri Kitwanga alizikagua nyumba hizo za zamani pamoja na zakisasa zilizopo katika eneo hilo.
 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiiangalia nyumba ya mabati ya makazi ya Polisi wakati alipoingia ndani huku akitokwa na jasho kutokana na joto kali ndani ya nyumba hiyo. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kutembelea nyumba hizo zilizopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na kushoto ni  mkazi wa nyumba hiyo, ambaye ni askari Polisi, Nelson Chale.
 

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kushoto) wakizikagua nyumba za kisasa ambazo ni za ghorofa za Jeshi ya Polisi nchini zilizopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara kuzitembelea nyumba hizo ili kujionea ukosefu wa nyumba unaowakabili Polisi nchini. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...