
Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.

Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).

Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo tarehe 28 Desemba 2015.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Kwa nini wizara hii ya mali asili isiongoze kwa kuwa na samani itengenezwayo na maliasili ya Tanzania na mafundi/nguvukazi(maliasili namba 1 ya taifa lolote)ya Tanzania, badala ya samani duni za nje? uko wapi uzalendo wetu? Vijana wetu mafundi wetu watapata wapi fursa ya kujenga na kuonyesha umahiri wao kama siyo kuanzia serikalini na katika taasisi za Kitanzania?
ReplyDelete