Washiriki wa Mafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini Mafunzo hayo..
Awamu ya Tatu ya Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanza leo. Wanawake 35 wa jiji la Dar es salaam Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Felix Maganjila na Shekha Nasser. Mafunzo hayo yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo
 Mafunzo haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake.
 Awamu ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali
 Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwana Mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa Lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimeyapenda Haya mafunzo na nayahitaji, ni lini tena yatafanyika hapa Dar?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...