Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said Suleiman amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea katika pwani ya Dar es salaam.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu, ambako baada ya kufikishwa ikaelezwa kuwa amekwishafariki.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Upanga jirani na Makao makuu ya JWTZ na mazishi yanmepangwa kufanyika saa kumi jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Marehemu alipata kuwa Katibu mkuu wa klabu ya Simba ambako kuitokana na uchapakazi wake akapachikwa jina la Yelstin.
Taarifa zaidi tutazidi kufahamishana kadiri ya zikavyokuwa zikiingia,kupitia hapa hapa Globu ya Jami.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...