Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
machine sawa na tunaishukuru sana serikali...
ReplyDeleteshida ni ma' nurse haswa nyakati za kuwahudumia wagonjwa kuna malalamiko meengi toka kwa wagonjwa kutelekezwa na ma'nurse.. naomba jambo hili liangaliwe kwa jicho la pili
Wewe mdau hapo juu, kama huyaridhika na utendaji kazi wao yakupaswa kumreport huyo nurse kwani anakuwa amevaa kitambulisho kinachoonesha jina lake. Hii ni kasi ya awamu ya tano.
ReplyDelete