Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour kati kati akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal (kushoto)  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi nyumbani kwake Kidombo mara baaya ya chakula cha mchana.
Hafla hiyo inayojumuisha mamia ya waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka pembe zote za Unguja huambatana pia na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Duniani Mtume Muhammad { SAW  } wakati wa usiku ukiwa ni utaratibu wa  Dr. Salmin kuandaa ifikapo Mfunguo Sita wa kila mwaka.
 Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj Ali Haasn Mwinyi (wa pili kutoka Kushoto)  akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (wa kwanza kutoka kushoto) na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia)  wakijumuika na waislamu katika Hitma ya kuwaombea dua Waumini waliotangulia mbele ya haki hapo Msikiti wa Ijumaa Kidombo Kijijini kwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Dr. Samlin Amour.
Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka sehemu mbali mbali Nchini wakihitimisha Hitma ya kuwaombea waislamu walitangulia mbele ya haki hapo kwenye Msiki wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja Kijiji alipozaliwa Rais Mstahafu wa Zanzibar Dr. Salmin Amour.
Picha na OMPR, ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...