Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Naibu Inspekta Generali wa Polisi, D/IGP Abdulrahman Kaniki wakati Katibu Mkuu huyo akiambatana na Naibu wake, Balozi Simba Yahya (wakwanza kushoto) walipokuwa wanawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katikati ya Katibu Mkuu na D/IGP ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ambaye alikuwa anawatambulisha viongozi wakuu wa jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (meza kuu kushoto) akiwaongoza viongozi wakuu wa Jeshi hilo kuimba wimbo wa maadili kabla ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (meza kuu katikati) pamoja na Naibu wake, Balozi Simba Yahya (kulia meza kuu) kuzungumza na viongozi hao wakati walipofanya ziara ya kikazi ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (wapili kushoto) akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) wakati Katibu Mkuu huyo ambaye aliambatana na Naibu wake, Balozi Simba Yahya (wapili kulia meza kuu) katika ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Meja Jenerali Rwegasira aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanaliondoa tatizo la kuwabambikizia kesi wananchi linalofanywa na baadhi ya askari wasiokuwa na maadili ndani ya jeshi hilo, kwa kuwa wanalitia doa jeshi hilo ambalo linasifa nzuri nchini na nje ya nchi. Kulia meza kuu ni Naibu Inspekta Generali wa Polisi, D/IGP Abdulrahman Kaniki na kushoto ni Kamishina wa fedha na Lojistiki wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...