Kutoka kushoto: Afisa tawala katika mahakama ya Wilaya ya Serengeti Faraja Barakasi, Hakimu Makazi Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile, Meneja Mahusiano wa Singita Grumeti Reserves na Grumeti Fund Ami Seki ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Serengeti(DED) Naomi Nnko, Katibu tawala wa Wilaya ya Serengeti(DAS) Cosmas Qamara, Laurian Lamatus ,Moremi Mrigo na Samson Ndeki ambao wa wote ni wafanyakazi wa Grumeti wakiwa katika halfa ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tehema vilivyotolewa na Grumeti kwa mahakama ya Wilaya ya Serengeti hivi karibuni
Na
Anthony Mayunga.
Mahakama ya Wilaya ya Serengeti imepokea msaada wa
vifaa vya kisasa vya tehama (ICT) ambavyo vimetolewa na kampuni ya utalii ya
Singita Grumeti Reserves na shirika lake dada la Grumeti Fund.
Vifaa hivyo ikiwemo kompyuta na printa vilikabidhiwa
mwishoni mwa wiki iliyopita kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Serengeti
Ismael Ngaile katika hafla iliyofanyika katika ofisi za mahakama hiyo iliyopo
mjini Mugumu.
Ngaile
alishukuru Grumeti kwa kuitikia ombi lao kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi
kuvitumia kuboresha huduma katika mahakama hiyo.
“Tulikuwa tunafanya kazi kwa kutumia computer moja
lakini sasa ufanisi utaongezeka na nakala za hukumu zitatoka mapema kuliko ilivyokuwa zamani. Hivyo kwakweli
tunashukuru sana ”,alisema Ngaile.
Meneja wa Mahusiano wa Singita Grumeti Reserves na Grumeti Fund Ami Seki alisema msaada huo ni sehemu tu ya mchango wanaotoa kuboresha huduma
mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda , Mkoani Mara.
“ Tuna amini
kuwa vifaa hivi vitasaidia kurahisisha kazi za kiofisi na hivyo
kuboresha huduma na hii ni sehemu tu ya
misaada inayotolewa na Singita Grumeti Reserves kwa kushirikiana na Grumeti
Fund kuboresha huduma kwa wananchi”, alisema Seki.
Akizungumza katika halfa hiyo, Katibu Tawala wa
Wilaya ya Serengeti (DAS) Cosmas Qamara alisema vifaa hivyo vitaiwezesha
mahakama hiyo kufanya kazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo
kuharakisha upatikanaji wa haki.
“Nina imani sasa wananchi watakuwa wanapata nakala
za hukumu ndani ya wiki moja badala ya miezi mitatu na ni hatua nzuri katika kupata haki kwa
wakati”, DAS Qamara alisema.
Alitumia fursa hiyo kuishukuru Grumeti kwa kuendelea
kutoa misaada mbalimbali ambayo inasadia kubadilisha maisha ya wananchi.
“Tunatadhamini sana juhudi mnazozifanya. Hii sio
mara ya kwanza kupata msaada kutoka kwenu (Grumeti). Mmefanya mambo mengi
mazuri katika sekta za elimu, maji na afya”, alisema Qamara.
Hafla hiyo pia ilihudhuria na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (DED) Naomi Nnko na Mwenyekiti wa Halmashuri
hiyo Juma Porini.
Viongozi hao pia walisema kampuni ya Grumeti
imeonesha mfano ambao unapaswa kuigwa na wawekazaji wengine ambao wamewekeza
katika wilaya hiyo.
“Grumeti ni wadau wetu muhimu sana. Wamefanya mambo mengi sana na
wadau wengine wajifunze kutoka kwao”, alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Serengeti Juma Porini.
Singita Grumeti Reserves Ltd ni kampuni ya kitalii
ambayo inaendesha hoteli kadhaa za kifahari katika mapori tengefu ya Grumeti na
Ikorongo yaliyopo Mkoani Mara . Hoteli hizo zinamilikiwa na Paul Tudor Jones,
ambaye ni mwekezaji kutoka Marekani.
Na Grumeti Fund ni shirika dada la Singita Grumeti
Reserves Ltd ambalo linashugulikia uhifadhi wa maendeleo ya jamii.
Uwekezaji katika miradi ya jamii ambao unafanywa na
Singita Grumeti Reserves kwa kushirikiana na Grumeti Fund unaripotiwa kupunguza
vitendo vya uwindaji katika mapori tengefu ya Ikorongo na Grumeti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...